Jumatatu 31 Agosti 2026 - 12:11
Bilal Muslim Temeke, Yaadhimisha Hafla ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

Hawza/ Kituo cha Bilal Muslim kimeandaa hafla maalumu ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), katika tukio lililolenga kuenzi maisha, ujumbe na mafundisho ya Mtume Mtukufu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi, tarehe 29 Agosti 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) yaliyowakutanisha waumini katika kumkumbuka na kumuenzi Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Maadhimisho hayo ilikuwa ni fursa muhimu ya kuwakumbusha waumini nafasi kubwa ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) katika kuiongoza jamii kuelekea katika misingi ya imani, maadili mema, upendo na mshikamano.

Kupitia maadhimisho hayo, Kituo cha Bilal Muslim kimeendelea kutoa nafasi kwa waumini kushiriki katika shughuli za kumuenzi Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na kutafakari mafundisho yake ambayo yanaendelea kuwa mwongozo muhimu katika maisha ya Waislamu.

Hafla hiyo ilifanyika katika mazingira ya furaha na kumuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w.), huku ikisisitiza umuhimu wa kuyafanya mafundisho yake kuwa sehemu ya maisha ya kila siku na msingi wa kujenga jamii yenye maadili, mshikamano na upendo.

Bilal Muslim Temeke, Yaadhimisha Hafla ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

Bilal Muslim Temeke, Yaadhimisha Hafla ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

Bilal Muslim Temeke, Yaadhimisha Hafla ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

Bilal Muslim Temeke, Yaadhimisha Hafla ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.)

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha